
Je siku hizi nimekuambia nakupenda
Kile tumechoambiwa na wazazi wetu kitakaa nasi kwa milele.
Watoto wanatakikana kusikia kama wanapendwa na kubaliwa vile wameumbwa, sio kwa ajili ya mambo wametenda vizuri au kazi wamefanya.
Kila mtoto ni tofauti na pekee
Thamini na shajiisha tofauti za kipekee za watoto.
Kila mtoto huruzuku mengi kwa familia, warafiki na jamuiya.
Watoto wanatakikana kujisikia vizuri
Kujiheshimu ni kusikia vizuri ukifikiria juu yako, na kujisikia kama uko azizi. Kujiheshimu hupatia mtoto imani na tamani kwa wakati wa ubele. Watoto wanatakikana kujipenda, kusikia kama wako muhimu, werevu na wanaweza kutekeleza mengi maishani mwao. Watoto ambao wanajiheshimu wako na tumaini kwa kujifunza na kujaribu kufanya mambo mapya.
Jinsi ya kuambia watoto umuhimu wao
Wambie mara nyingi unawapenda vile wameumbwa.
Unaweza kuwaonyesha unawapenda ukitoa wakati wa kushinda nao, ukisikia maneno yao na kuwambatiana nao na kucheka nao.
Sherekea matekelezo yao, hata kama ni ndogo.
Wasifu wakijaribu, usilinganishe matokeo ya kile wanachofanya.
Weka makumbusho spesheli ya mafanikio na hatua yao.
Wakitaka kukusaidia wapatie nafasi.
Wajulishe ni sawa kufanya makosa. Kile wanachofanya kinawasaidia kujifunza.
Wasaidie kujenga vipaji vyao.
Waulize fikira zao juu ya mambo yanayofanyika kwa jamii. Hii itawaonyesha unajali vile wanafikiria.
Wasaidie kusululisha matatizo yao. Waonyeshe uko na imani nao.
Lingana na bainisha mifiko na matarajio yako.
Watolee marudio juu ya miendo yao ambaye sio sawa lakini usiwahukumu.
Dhamira ya marudio ni kufundisha mtoto yako si kumumiza.









